Ads 468x60px

Jul 2, 2013

FIQ-HI na umuhimu wake - PT 1‏ (Kiswahili)


Assalaamu alaikum,
 Natumai hamjambo. Wakati tunajiandaa kumkaribisha mgeni wetu mtukufu, nimeona bora nilete mada moja nyeti kwani wengi wa vijana wetu leo wanapumbazwa nalo na hivyo hujiharibia mwelekeo wa Uislamu.
 AYA:  YA AYYUHALLADHINA AMANU ATI-ULLAHA WA ATI-UR RASUL WA ULIL AMRI MINKUM.
Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam, aya hapo juu ya Sura An Nisaa 4: 59 inayozungumzia uhakika wa fiq-hi au maarifa ya sheria za Kiislamu na ndiyo itakuwa mada yetu leo kwani wengi wa ndugu zetu hawana elimu nayo.
Uthibitisho wa fiq-hi ndani ya Quran; TAFSIRI: Enyi mlioamini mtiini Allah na mtiini Mtume na wenye kuwa na amri juu yenu.
Kwanza kabisa ieleweke kuwa kuna njia 4 za kufuatwa katika kutatua masuala ya dini, nazo ni : Quran, Hadithi, umoja wa Ummah na kukisia.
Nini maana ya FIQ-HI? Fiq-hi ni falsafa ya sharia za Kiislamu na inaelezea sharia za dini kupitia Quran na Sunnah (Hadithi).  Mfano wake ni kama khalifa au mfalme atoe hukumu kwa kuzingatia sheria ya dini, na khalifa au mfalme huyo akitenda kinyume na sheria, basi huyo hatafuatwa. Mfano: Sy AbuBakr alipokuwa khalifa, aliwauliza Masahaba: enyi watu, mimi ninapofuata amri ya Allah na Mtume wake ni sawa, je ikiwa nikienda kinyuma mtafanyaje? Sahaba mmoja masikini alisema: tunaapa kwa Mola aliyetuumba, tutakunyoosha kama mkuki. Ndipo Sy AbuBakr aliwaambia : nyinyi ni waelewa.
Pia tuna maimamu wanne au madhehebu nne za kufuata sharia za Kiislamu nazo ni Imam Abu Hanifa, Imam Shafi’I, Imam Ahmad bin Hambal na Imam Malik Rahimahumullah.
Nini maana ya umoja wa ummah? Mfano Qadhi atatoa hukumu kutokana na kauli za Masahaba.
Nini maana ya kukisia? Ni kauli au hukumu za Masahaba, Tabii na Maimamu wanne. Yule asiyewakubali hao basi mfano wake ni kama mwenye kuumwa na tumbo kisha akadai kuwa akienda kwa daktari basi ataingia gharama maabara na mengineyo. Ni bora tu anunue dawa ya tumbo dukani na atapona!! Na ndiyo maana watu kama hao ni wapotovu.

Maswali / maoni yanakaribishwa. Pia kama una mada yoyote unataka itumwe risala yake, basi naomba tu usisite na mimi in sha Allah nitajitahidi kuizungumzia.
JazakAllah,
Muhammad KHATRI 

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views