Ads 468x60px

Jul 5, 2013

FIQ-HI na umuhimu wake - PT 2 (MWISHO)‏ (Kiswahili)


Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo. Ijumaa Kareem. Mtaniwia radhi ila wakati mwingine nakuwa na wasiwasi kuwa hivi kweli inawezekana isizuke swali hata moja katika risala zote hizo ninazotuma!!!!
Nawaombeni msisite ndugu zangu, kwani mimi huwa simtaji yeyote katika risala zangu na hivyo swali linaloulizwa inakuwa ni siri yang utu, usihofu!
AYA:  YA AYYUHALLADHINA AMANU ATI-ULLAHA WA ATI-UR RASUL WA ULIL AMRI MINKUM.
Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam, aya hapo juu ya Sura An Nisaa 4: 59 inayoelezea umuhimu wa Fiq-hi na leo tutazungumzia kuhusu ukisiaji wa mjinga na wa mjuzi.
Tulizungumzia kuhusu uthibitisho wa fiq-hi ndani ya Quran; TAFSIRI: Enyi mlioamini mtiini Allah na mtiini Mtume na wenye kuwa na amri juu yenu.
Swali linakuja, je Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam amezungumzia nini kuhusu hilo?
Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alimtuma Muaz bin Jabal kuwa Qadhi wa Yemen, ila kwanza alimuuliza kuwa atahukumu vipi kesi atakazoletewa? Muaz alijibu kuwa kwanza ataangalia ndani ya Quran, kisha Hadithi. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alimuuliza kuwa je kama hukufanikiwa kupata jibu ndani ya Quran na Hadithi, hapo utafanyaje? Muaz alijibu kuwa katika hali hiyo atakisia akizingatia mafundisho ya Quran na Hadithi. Ndipo Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alimshukuru Allah kuwa watu wa aina hiyo wapo katika umma wake.
Tuangalie ukisiaji wa mjinga na mjuzi: Bwana 1 alipanda juu ya mti lakini alishindwa kushuka huku watu wakimsubiri chini. Mara akapita mpita njia na alipoona hivo aliwashauri wamrushie kamba kisha yule bwana aiufunge kiunoni ndipo waliopo chini wamvute, kwa hali hiyo atashuka kirahisi tu. Walipomvuta, yule bwana akaanguka na kufa papo hapo.Ndugu zake walianza kumhoji yule mpita njia, ambae alijitetea kuwa eti ni juzi tu alimtoa mtu 1 kutoka kisimani kwa staili hiyo na alinusurika!! Hivi ndivyo wajinga wanavyokisia.
Kuwaamini maimamu wote wanne (Imam Abu Hanifa, Imam Shafi, Imam Malik na Imam Ahmad bin Hambal) na kumfuata mmojawapo ni jambo la lazima. Pia siyo kuwa baadhi ya masuala amfuate imam mmoja na baadhi amfuate imam mwingine. Mfano wa mwenye kufanya hivyo ni kama mgonjwa wa tumbo akatafuta tiba kwa madaktari wanne tofauti, hivyo hali atakayokuwa nayo mgonjwa huyo ndivyo atakuwa mwenye kuwafuata maimamu tofauti.
Ila kama kuna dharura ndipo anaweza kumfuata Imamu mwingine. Mfano: kwa Imam Shafi mtu akimgusa mwanamke basi udhu wake hubatilika, hivyo wakati wa kutufu Al Ka-aba wanamfuata Imam Abu Hanifa.
Masahaba walipokuwa na tatizo lolote basi walimwendea Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam, lakini je baada ya yeye kuiaga dunia?
Kwa Sy AbuBakr, ikamfikia kesi moja na suluhisho yake haikupatikana ndani ya Qurani wala Hadithi. Kisha aliwauliza Masahaba: je mnakumbuka kuwa kesi kama hiyo ilimfikia Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam na alijibu nini? Masahaba walijibu: ndiyo tunakumbuka na Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alijibu hivi. Sy AbuBakr akatoa hukumu juu ya suala hilo kisha alimtukuza Allah na kumshukuru kwa kusema kuwa wapo waja wako ambao hata na leo pia wanakumbuka kauli ya Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam.
Tuangalie ukusiaji wa wajuzi: kwa Imam Abu Hanifa alikuja bwana 1 na kumuambia: nimetenda kosa 1, nimewajibika kuoga ila katika kugombana na mke wangu kuwa ikiwa nitaoga basi mke wangu awe na talaka 3!! Sasa wanaosema tufuate Qurani na Hadithi tu, walete aya au Hadithi inayotoa hukumu ya kesi kama hiyo!! HAKUNA. Imam Abu Hanifa kamwambia afuatane nae na walipofika kando ya mto, Imam alimsukuma hadi yule bwana katumbukia kwenye mto. Alitoka kwa shida, ila mke wake alisalimika na talaka kwani kwa kutumbikia kwenye maji ina maana alijiogea bila ya kutarajia. 
Majambazi 4 walipora mali kisha wakwamwambia kuwa kama yeye atawashitaki kuwa fulani na fulani ni mwizi, basi mkewe atakuwa na talaka 3. Kwa hali hiyo aliyeporwa hakuwa na jinsi ila kunyamaza tu huku majambazi walitamba mitaani bila kushitakiwa. Baada ya masiku aliambiwa amwone Imam Abu Hanifa. Akamwelezea tatizo lake, Imam akamwambia awaalike majambazi wote, pia wakaandaliwa wababe kama 5. Wababe walisimama mlangoni baada ya karamu na kila jambazi akitoka yule aliyeibiwa aliulizwa: je huyu ndiye jambazi? Akitoka jambazi asiyehusika na tukio la kumpora, yule bwana alijibu : siye; ila kwa wale wane aliambiwa akae kimya na wale wababe wataelewa na kuwakamata. Kwa hali hiyo majambazi wote 4 walikamta, mali yake ikapatikana na mkewe kusalimika na talaka 3.

In sha Allah wiki ijayo nitaanza risala za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Maoni / maswali yanakaribishwa.
JazakAllah,
Muhammad KHATRI 

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views