Ads 468x60px

Jul 25, 2013

RAMADHAN KAREEM - PT 6 (JIHAD)‏ (KISWAHILI)


Assalaamu alaikum,

Natumai hamjambo na mnaendelea na ibada ya swaum pamoja na ibada zingine.
Mwezi 17 ya Mfungo huu wa Ramadhani, vita vya kwanza vilitokea huko Badri.

AYA: YA AYYUHALLADHINA MANU HAL ADULLUKUM ALAA TIJARATIN TUNJIYKUM MIN ADHABIN ALIM. TU-UMINUNA BILLAHI WARASULIH, WATUJAHIDUNA FI SABILILLAHI BI-AMWALIKUM WA-ANFUSIKUM, DHALIKUM KHAIRULLAKUM IN KUNTUM TA-ALAMUN.
Baada ya Kumshukuru Allah na kumtakia Rehma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam, hapo juu ni aya ya 10 na 11 ya Sura As-Swaaf kutoka Quran inayozungumzia jihad na ndiyo itakuwa mada yetu.
Tunaendelea na mwezi Mtukufu wa Ramadhani, mwezi ambamo mambo kadhaa yamedhihirika. Ni katika mwezi huu saumu ikafaradhishwa, qiyam ya usiku yaani sala ya tarawih ikawekwa ni jambo la thawabu, ni mwezi wa kuomba dua na ni mwezi ambamo dua inakubalika. Pia ni mwezi ambamo mna usiku wa Lailatul Qadri. Fadhila nyingine ni kuwa Quran imetelemshwa katika mwezi huu.
Wafasiri na wanazuoni wakuu wanaelezea kuwa vitabu vyote vya mbinguni vimeteleshwa katika mwezi huu.
Ni katika mwezi huu katika maeneo ya Badri, vita kati ya Waislamu na makafiri, iitwayo vita vya Badri, ilitokea ambayo ilidhihirisha ujasiri wa Uislamu. Makafiri walidhalilika mno na hawakutegemea kabisa. Hivyo leo tutazungumzia kuhusu vita vya Badri ili kujipatia thawabu za kuwakumbuka Masahaba mashujaa waliojitolea kwa hali na mali kuitetea Uislamu.
Tafsiri ya aya: Enyi mloamini, je Nisiwaonyeshe biashara itakayowaokoa na adhabu kali? Muaminini Allah na Mtume Wake, na piganeni jihad katika njia ya Allah, kwa mali yenu na nafsi zenu, haya ni bora kwenu ikiwa mnafahamu. (SURA: AS-SWAFF: 10-11)
Biashara ni jambo ambalo inampatia mtu faida. Hapa Allah Anazungumzia kuleta imani juu ya Allah na Mtume Wake, kusoma kalima, ndipo itamletea mtu faida; vinginevyo hatapata faida yoyote. Kisha Allah akaagiza jihad katika njia Yake kwa mali na nafsi zetu; na hii akaitaja kuwa ni bora kwetu.
Hivi sasa Waisalmu wanadhalilika ulimwenguni ni kwa sababu ya kuacha jihad. Pili mali na pesa imewafanya watu kuwa waoga. Tatu jihad huzidisha hadhi ya Uislamu. Uislamu ni dini ya amani, lakini pindi inapoandamwa kutaka kuangamizwa, basi ni vyema ikahifadhiwa kwa jihad. Anaeuawa katika jihad ni shahidi. Pia anaejeruhiwa katika jihad, basi siku ya kiyama damu itatoa ushahidi wa kunukia kama zafarani. Shahidi hataogeshwa bali atakafiniwa katika nguo zenye damu, atasaliwa jeneza na kuzikwa. Siku ya kiyama atafufuliwa na nguo zake za damu. 
Hadithi: Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam amesema kuwa mtu mwenye macho aina mbili hataingia motoni. Moja: ni mwenye kutokwa na machozi katika hofu ya Allah na PILI macho yaliyokesha wakati wa jihadi ikichunga uvamizi wa adui.
Hadithi: Mtu huyu hataingia motoni ambae miguu yake ikapatwa na vumbi katika njia ya Allah.

Maswali / maoni yanakaribishwa.

JazakAllah,

Muhammad KHATRI

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views