Ads 468x60px

Jul 28, 2013

RAMADHAN KAREEM - PT 8 (SWALI / JIBU)‏ (KISWAHILI)


Assalaamu alaikum,

Natumai hamjambo na mnaendelea na ibada ya swaum pamoja na ibada zingine.
Kuna ndugu yetu ameandika maoni yake na kuuliza swali pia, na kama ilivyo ada yangu, huwa simtaji muulizaji. Maoni/ swali ni hii ...

SWALI: Leo nina maoni tu na kama nitakosea naomba unirekebishe Inshaallah nia ni kuipeleka mbele Dini hii tukufu ambayo ndio njia sahihi ya kuiendea Jannah ya Allah. Tumesisitizwa sana kwamba tunapohitilafiana turudi kwenye kitabu kitakatifu Qur an pamoja na Sunna za Mtume wetu Muhammad (SAW). Mimi sijakubaliana na ushauri ulioutoa wa kuwahusia waislam kutokuswali katika misikiti ya Answar Sunnah.
Mimi naamini sisi kama waislam tumesisitizwa sana kwenye suala la umoja(Tushikamane kwenye kamba moja na tusifarakane), na umoja ndio ambao utatuletea maelewano miongoni mwetu na kuwa na mawasiliano mazuri. Je ni vipi utaweza kumuelimisha Yule ambaye unaona anakosea wakati unamkimbia, Je nini hukumu ya Yule anayesikia Adhana kwenye msikiti uliokaribu na kuenda msikiti wa mbali kwa ajili ya sala na baadae kurudi hapo alipo? Kama nilivyotangulia kubainisha mwanzo tumehimizwa njia za kuziendea Khilafu zilizopo, badala ya kumkimbia mtu muelimishe kwa nini anachofikiria au anachokifanya sio sahihi kwa kutumia Aya za Qur an na Hadith za Mtume(SAW).
Hiyo peke yake ni mada tofauti na ina malumbano yasiyoisha!! Answar Sunnah (kwa hapa Afrika Mashariki), wahabi (sehemu nyingi duniani), Ahlul Hadith (sehemu kubwa ya Bara Hindi), Salafi (sehemu kubwa ya Uarabuni) ni baadhi tu ya majina yamebuniwa na vikundi hivyo - wote wakiwa na lengo takriban moja tu. Mwanzilishi mkuu alikuwa Muhammad ibn AbdulWahab wa Najdi (sasa Riyadh) Saudia. Siri zake za jinsi alivyonunuliwa na waingereza ili tu kuleta mfarakano miongoni mwa Waislamu na Usilamu kwa ujumla na hasa kupunguza mapenzi ya Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam katika mioyo ya Waislamu, unaweza kuzisoma katika kitabu "Confessions of a British Spy", ambacho nimeambatanisha kwa faida na manufaa yetu sote.
Kwa muhutasari tu, licha ya kusomewa Aya za Quran Tukufu au Hadithi, lakini bado wanashikilia msimamo wao ili kutekeleza matakwa ya vibaraka zao!! Kusali pamoja nao kuna madhara ya kuwa wengine nao watadhani kuwa "huyo nae ni miongoni mwao!!" Ni sawa na kusema mimi nimeingia baa labda kununua soda, ila nitadhaniwa pengine ni "mnywaji"!! Ndyo maana wanazuoni wamesema ni bora kujiepusha.
Vile vile tukumbuke Hadithi ya Mtume : "ummah wangu itagawanyika katika makundi 73, vyote vitakuwa vya motoni isipokuwa moja tu". Hivyo kauli ya Mtume haitakuwa ya uongo abadan!!

Naamini tukianza utengano huu hautishia hapo, kwani tutasema tusiswali kwenye misikiti ya Ibadh, lakini sio hilo tu tusisali na wale wanaofungia sala kifuani, au wanaofungia chini ya kifua au wasiofunga mikono kwenye sala, pia wale wanaotoa salam moja baada ya Shahad ya mwisho na vile vile wale wanaokunut nawale wasiokunuti. Tutaanza utengano misikiti na miskiti lakini haitaishia hapo tutakuja kati ya waumini ndani ya msikiti mmoja(je hatujaona au kusikia misikiti ikiswali jamaa mbili kwa mara moja kutokana na misimamo tofauti?) na mwisho tutaishia kati ya muumini na muumini.

Ikiwa Muislamu anatekeleza / kufuata kanuni ya mmojawapo kati ya Maimamu wanne, basi yumo kwenye njia sahihi.

Kwa uelewa wangu mdogo tofauti zetu kubwa zimekuwa kwenye mambo ya Sunnah tunapoongelea mambo ya fardhi tunakuwa pamoja. Nafikiri cha muhimu kwenu wanazuoni kutuelimisha sisi maamuma na sisi maamuma vile vile kufanya jitihada ya kuijua Dini yetu tukufu kwa njia mbalimbali na kuacha kusema mimi tu nilisikia kwa shehe huyu au shekhe Yule, Allah ametupa akili tufanyie kazi yote yanayotuijia(simaaninishi tusiwasikilze Mashekhe zetu bali tujaribu kupima tunayoyapata kwa akili zetu) maana kila mtu atahukumiwa kivyake. Tuna vita kubwa ya kuhakikisha kwanza kabisa kwenye Umma huu wa uislam tunao ndugu zetu wengi sana ambao hata hawatekelezi nguzo muhimu ya Sala, na hao wanaachwa tunasema shauri zao, tutakuja ulizwa kuhusu hilo. Tunaondugu zetu wengi wanaokubali kuitwa wageni misikitini kila mwaka, maana inapokaribia Ramadhani utasikia jamani tujiandae kuwapokea wageni miskitini na Ramadhani ikiisha wanaondoka, tuwafanyie kazi hawa wabaki misikitini. Hebu tujiulize ndugu zangu uingie nyumbani kwako halafu mwanao amwite mkeo anamuambia mama kuna mgeni amekuja sababu hakuoni nyumbani utajisikiaje, ndugu zangu waislam Misikiti ndio nyumba zetu za ibada tuipambe kwa kuijaza muda wote wa mwaka na sio Ramadhani,Ijumaa na siku ya saal za Eid tu.
NB: Nilikuwepo kwenye hutba moja ya ijumaa Ramadhani ya mwaka jana kwenye msikiti wa Vetenary kwa sheikh Kishki, mada ilikuwa ni ipi idadi kamili rakaa za salat Taraweh(huwa anakuwa na CD anauza lakini wametengeneza kitabu kidogo kutokana na hutba hii,unaweza vitafuata), nilifurahi sababu alijitahidi kuelezea vizuri kuhusu pande hizi mbili na Hadith wanazosimamia. Lakini pamoja na kuonyesha msimamo wake ni upi, ushauri wake ulikuwa kwamba ukiswali kwenye msikiti wanaosali rakaa 20 hakikisha unasali na imamu mpaka mwisho nausikatishe kwa sababu kuna faida kubwa kuanza na kumaliza na imamu na hata ukiswali kwenye msikiti wa naosali rakaa nane hivyo hiyo.

Nimepata kusikia sifa za huyu shekhe, ila sielewi kama alijaribu tu kutowakasirisha wanaosali rakaa 8 au vipi. Ila wanazuoni wanasema mwenye kusali rakaa 8 anaenda kinyume na mafundisho ya Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam na baya zaidi anadanganya kwani rakaa 8 ni tahajjud na sio taraweh!!

Samahani kwa kukuchosha kwa maelezo mengi hii inatokana na elimu ndogo, naomba kusahihishwa nilipokosea.

JIBU: Kwanza kabisa naomba nieleweke kuwa mimi si shekhe ila pengine kwa sababu tu napendelea kutoa risala kutokana na mafundisho ninayoyapata, basi wengi hudhani mimi ni shekhe; hivyo kukosea/ kuteleza katika maoni ni jambo la kawaida.
Pia kutokana na urefu wa maoni/ swali, nimejaribu kujibu baada ya paragraph ya swali hapo kwa wino mwekundu.
Natumai nimejaribu kuchambua swali / maoni, ila kama bado kuna dosari basi nitafurahi kuambiwa ili tujaribu kuelimishana.


Maswali / maoni yanakaribishwa.

JazakAllah,
Muhammad KHATRI 

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views