Ads 468x60px

Jul 22, 2013

RAMADHAN KAREEM - PT 4‏ (KISWAHILI)


Assalamu Alaikum 

Natumai hamjambo na mnaendelea na kumi za kati za Mfungo wa Ramadhan. Tunaendelea na risala yetu...

Baada ya Kumshukuru Allah na kumtakia Rehma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam, leo Insha Allah tutazungumzia kuhusiana na mambo yanayo batilisha saumu.
 1)  Mwenye kula, kunywa au kumuingilia mke katika hali ya kuwa anafahamu kuwa yumo ndani ya saumu, vinginevyo saumu haitabatilika.
 2Mwenye kuvuta sigara, kiko na vinavyo fanana navyo vya kuvuta.
 3 Mwenye kutafuna tambuu au tumbaku hata kama atatema.
 4)  Mwenye kuweka sukari, pipi, n.k. mdomoni kisha ikayeyuka na akameza mate yenye ladha ya vitu hivyo.
 5)    Kama kulikuwa na kitu kimenasa kwenye meno yenye ukubwa mfano wa mbegu ya maharage, ukakimeza, au kilikuwa ndogo ya hapo ila ukaitoa kisha ukaimeza itabatilisha saumu. Pia ukatokwa na damu kwenye meno mfano wa mate na ukahisi ladha ya hiyo damu itabatilisha saumu.
 6)    Matumizi ya sindano au ukaweka dawa puani au masikioni au ukatia mafuta masikioni itabatilisha saumu. Maji yakiingia masikioni haitaleta madhara kwa saumu.
 7)    Ulikuwa ukisukutua na bahati mbaya maji yakavuka koo au ulikuwa ukisafisha pua na maji yakavuka hadi kuelekea kwenye bongo basi itabatilisha saumu. Hata hivyo kama ulikuwa hufahamu kuwa umo ndani ya saumu basi haitabatilisha.
Maswali / maoni yanakaribishwa. 
JazakAllah,
Muhammad KHATRI

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views