Ads 468x60px

Sep 10, 2013

MTUME IBRAHIM - PT 2‏ (KISWAHILI)


Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo.
Tunaendelea na risala juu ya maisha ya Mtume Ibrahim Alaihissalaam.
AYA:  ALAMTARA ILALLADHI HAAJJA IBRAHIMA FI RABBIHI AN AATAHULLAHUL MULK.
Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam, imesomwa kipande cha aya 258 ya Sura Baqara, inayozungumzia Mtume Ibrahim Alaihissalaam.
Mtume Ibrahim alikabiliana na ufalme wa Namrud. Ikumbukwe kuwa Azar aliyetajwa ndani Quran na aliyekuwa mshirikina akiabudu masanamu, si mzazi wa Ibrahim bali ni ami wake. Mzazi wa Mtume Ibrahim anaitwa Tarikh bin Naakhur, aliyekuwa Muislam. Pia wazazi wa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam walikuwa Waislamu.
HADITHI: Mtume Swallallahu ALaihi Wasallam amesema kuwa: mimi ni Mtume na Mpendwa wa Allah, mimi ni mbora kwenu kwa kila hali; Allah Kaigawa dunia hii sehemu 2 – Uarabu na uajemi, Uarabu ukapewa ubora na mimi ni Mwarabu. Katika Uarabu kuna kabila nyingi na bora ni Quraish na hivyo mimi ni Mquraish. Katika Maquraish, kuna ukoo nyingi, bora ni Bani Hashim na mimi nimetokana na Bani Hashim. Bani Hashim ina familia nyingi na mimi katika familia Abdullah. Na eleweni kuwa mimi nimetoka kwenye mgongo ilitwahirika kutoka Mtume Adam hadi wazazi wangu Abdullah na Amina.
Mtume Ibrahim alizaliwa huku mzazi wake alishaiaga dunia hii na hivyo alilelewa na Azar. Azar na wakazi wote walikuwa wakiabudu masanamu na Namrud wakiamuamini kama mungu wao. Ieleweke kuwa Mtume anazaliwa tu tayari akiwa Mtume na hivyo anakuwa na maarifa ya Allah. Tangu utotoni, alipowaona Azar na wenzake wakiabudu masanamu, Mtume Ibrahim huchukia sana moyoni na alitafuta jinsi ya kuvunja masanamu.

Maswali / maoni yanakaribishwa
JazakAllah,
Muhammad KHATRI 

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views