Ads 468x60px

Feb 19, 2014

Shaikh AbdulQadir Jilani - PT 1 (Kiswahili)

Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo. Mtaniwia radhi kwanza kwa kimya kirefu na pili kwa kukosekana kwa tafsiri ya Qasida Burdah.
Mfungo tuliyonao ni wa Saba (Rabi-ul-Akhar), ambamo kiongozi wa Mawalii (Masharifu) – Shaikh Sayyid AbdulQadir Jilani RadwiyAllahu Anhu – aliiaga dunia. Ifuatayo ni sehemu ya kwanza ya risala fupi.




Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam, imesomwa aya ya Sura Yunus, inayozungumzia mawalii wa Allah na ndiyo itakuwa mada yetu leo kwani huu ni Mfungo 7 au Rabi ul Akhar, ambamo kiongozi wa Mawalii, Sheikh AbdulQadir Jilani aliiaga dunia.
AYA: Jihadharini, marafiki wa Allah hawana hofu wala huzuni.
                      
Baba yake, Abu Saleh, alikuwa Walii na Mcha Mungu sana. Hukaa kwa siku kadhaa ndani ya pango bila ya kula na kufanya ibada ya Allah. Siku moja alishikwa na njaa na hivyo kuanza kutembea kando ya mto kutafuta chakula. Aliona tunda ikielea na kuiila. Mara nafsi yake ikamuuliza lau kama mmiliki wa tunda hilo akimuuliza siku ya Kiyama kuhusu kulak wake bila ya kuomba, je atajibu nini? Hivyo akaanza kumtafuta mmiliki hadi kufika kwenye bustani la matunda na kumuomba msamaha mmiliki wa bustani, Abdullah Somai, ambae alikuwa Walii pia. Mmiliki alimpangia masharti mawili ili amsamehe; 1 – aihudumie bustani lake lote kwa miaka 10 na baada ya hapo ndipo aambiwe sharti la pili. Abu Saleh alikubali kuhofia shitaka siku ya kiyama. Baada ya miaka 10, Abu Saleh aliongezewa miaka miwili tena na baada ya miaka hizo miwili, aliambiwa kumuoa binti wa mmiliki aliye kilema wa macho, mdomo, masikio, mikono na hata miguu!! Sharti hili ilikuwa ngumu sana lakini Abu Saleh aliikubali pia. Siku ya kuonana na mke wake, alipoingia chumbani na kumsalimia, mkewe alimjibu. Abu Saleh mara moja alitoka nje ya chumba akidhani kuwa amekosea chumba! Baba mkwe alimwambia hajakosea chumba na aliyejibu salamu yake ndiye mkewe aitwae Ummul Kheir Fatima. Alimwambia kuwa binti wake kuwa kilema wa macho, mdomo, masikio, mikono na miguu alimaanisha hajawahi kutenda madhambi. Kutokana na wacha Mungu hao ndipo alizaliwa Sh AbdulQadir.

Maswali / maoni yanakaribishwa.

JazakAllah,

Muhammad KHATRI 

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views