Ads 468x60px

Jun 2, 2014

Mi-iraj - PT 3‏ (Kiswahili)

Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo. Tunaendelea na risala yetu kuhusu msafara wa Isra na Mi-‘iraj.
Baada ya Kumshukuru Allah na kumtakia Rehma Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam, hapo juu ni aya ya kwanza ya Sura Bani Israil, ambayo inazungumzia msafara wa miraji.
Tafsiri ya aya:
Utukufu ni Wake Yeye Aliyempeleka Mja Wake katika sehemu tu ya usiku kutoka Msikiti wa Haraam (Makkah) hadi Msikiti wa Aqsa (Palestina), ambao umezungukwa na Baraka Zetu, ili Tumuonyeshe baadhi ya alama zetu. Hakika Allah ndiye Mwenye Kusikia Mwenye Kuona.
Imeelezwa kwenye vitabu vya Bukhari na Muslim kuhusiana na msafara huo kuwa Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam alikuwa nyumbani kwa Ummi Haani, kisha aliletwa sehemu inaitwa Hatim ndani ya Msikiti Mtukufu wa Makkah. Hapa alipasuliwa kifua, moyo ulitolewa na kuoshwa na maji matukufu ya zamzam na kujazwa hikma ndani yake na kisha kurudishwa na baada ya hapo kifua kikashonwa. Baada ya hapo Malaika mtukufu Jibrail Alaihissalaam alimuambia kuwa Allah Amemuita. Aliletwa mnyama mmoja aitwae Burraaq, ambae ni mkumbwa kuliko punda na mdogo kuliko farasi, aliye na kasi kiasi cha kuwa hatua yake moja umbali wake ni sawa na tamati ya sisi kuona. Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam alimpanda na kuanza safari ya kwenda Msikiti wa Aqsa.
Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam alionyeshwa baadhi ya alama wakati anaelekea Msikiti wa Aqsa, nazo ni kama ifuatavyo:
1)    Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam aliwaona baadhi ya watu wakilima, huku wanaendelea kupanda mbegu na papo hapo mazao yalikamilika na watu hao kuvuna na kupata faida. Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam alifahamu kila kitu, lakini kuuliza kwake ni kwa ajili ya mafundisho kwetu.
Aliuliza: hivi ni kina nani hao?
Jibrail alimjibu: hawa ni katika ummah wako wanaotoa katika njia ya Allah; mfano kujenga Misikiti, madrasa, nk basi hupata faida papo hapo tu.
2)    Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam aliwaona watu wamelala na vichwa vyao kupondwa, kisha husima wakiwa wazima na baadae hulala na vichwa hupondwa.
Aliuliza: ni kina nani hao:
Jibrail almijibu: hao ni wale wanaopendelea kulala wakati wa sala ya Alfajiri, wanaona usingizi mtamu na pia huacha sala. Wataadhibiwa hivyo hadi siku ya Kiyama.
3)    Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam aliwaona baadhi ya watu wakila mawe na miti porini lakini hawashibi.
Aliuliza: ni kina nani hao?
Jibrail alimjibu: hao ni wale wasiotoa zaka kutokana na walichojaaliwa na Allah na pia hula haki za masikini.
Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam amesema kuwa toeni zaka ili mkinge mali zenu.
4)    Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam aliwaona watu ambao wamewekewa vyakula mbalimbali halali na vizuri sana mbele yao, lakini wanayaacha hayo na kukimbilia kula vyakula vibaya vilivyooza na kutoa herufu mbaya.
Aliuliza: ni kina nani hao?
Jibrail alimjibu: hao ni wale wanaowaacha wake zao halali na hukimbilia kwa wanawake wa nje na kutenda mambo ya haramu.
5)    Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam alimuona mtu mmoja mwembamba sana aliyekusanya kuni nyingi. Alipotaka kuubeba akashindwa. Badala ya kupunguza kuni kidogo, akaenda porini kuongeza kuni zingine.
Aliuliza: ni nani huyo?
Jibrail alimjibu: ni yule mwenye kuleta khiyana kwenye amana za watu na pia huweka tamaa apewe amana zaidi.
6)    Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam aliwaona baadhi ya watu wakikata taya zao kwa kisu kikali. Wanapomaliza za upande wa kulia na kukata za upande wa kushoto, za kulia huwa sawa.
Aliuliza: ni kina nani hao?
Jibrail alimjibu: hao ni wale wanaoeneza fitina kwa ulimi wao.
Hizo ni baadhi alama alizoonyeshwa Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam katika msafara wake..
Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah, 
Muhammad KHATRI

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views

Follow by Email