Ads 468x60px

Jun 5, 2014

Mi-iraj - PT 6 (MWISHO)‏ (Kiswahili)

Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo. Namalizia risala yetu kuhusu msafara wa Isra na Mi-‘iraj. In sha Allah risala ya mwezi Sha-‘abaan itafuata.
Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam, ilisomwa aya ya 8 HADI 10 ya Sura Najmi, inayozungumzia Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam kuonana na Allah.
Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam alishuhudia Pepo na moto na baadae kufika Sidrah, ambapo alisikia sauti ya SUB-HANALLAH, ALHAMDULILLAH. Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam aliuliza ni kitu gani hiyo? Jibrail akajibu kuwa Sidrah, ambayo ni mti mkubwa, Malaika huleta dhikri. Hapo ndipo tamati ya Malaika. Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam alimwambia Jibrail waendelee lakini Jabirail akamjibu kuwa akisogea hatua moja kutoka hapa basi mbawa zake zitaungua kutokana na Nuru ya Allah; akamuambia Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam aendelee na safari.
Hapa ndipo Jibrail alimuomba idhini Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam ili amuonyeshe utukufu aliojaaliwa na Allah; kwani siku zote hizo Jibrail alikuwa akimjia Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam katika sura ya binadamu tu. Jibrail alipoondoa pazia mbawa zake 600 zikaonekana na ukubwa wa kila mbawa ulizidi hata ukubwa wa ardhi yote ya dunia. Wanazuoni wanasema lau kama Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam angemuonyesha utukufu wake, basi Jibrail angezimia pengine hadi kiyama.
Baada ya hapo Jibrail alimuomba Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam amtakie idhini kutoka kwa Allah kuwa siku ya kiyama wakati umma wake utakapopita kwenye njia nyepesi, basi yeye atande mbawa zake kuwasalimisha wapite kwa raha.
Baada ya hapo Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam alimpanda Rafraf na kuelekea juu zaidi. Baada ya kupita Arshi ndipo alimuona na Allah kwa macho yake, na hapo ndipo alimkaribia Allah. Kisha Allah Alimjaalia wahyi. Allah Alimuuliza je umeleta nini?
Mtume : Attahiyatu lillahi wasswalawaatu wattayyibaatu.
Allah : Assalaamu alaika ayyuhan Nabiyyu warahmatullahi wabarakaatuhu (salamu ziwe juu yako ewe Mtume pamoja na Rahma na Baraka).
Mtume : Assalaamu alaina wa-alaa ibadillahis swaalihin (salamu ziwe juu yetu na waja wako wema).
Hapo ndipo Allah Alimzawadia sala 50 za kutwa nzima. Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam alianza safari ya kurudi, lakini alipokutana na Mtume Musa katika mbingu ya 6, alimuambia arudi kwa Allah ili zipunguzwe kwani ummah wake walifaradhishiwa sala 2 tu kutwa nzima na walishindwa. Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam alirudi tena kwa Allah kutaka kupunguziwa, na Allah alimpunguzia sala 5. Alipofika tena kwa Mtume Musa, aliambiwa bado ni nyingi na kurudi tena kwa Allah. Kila nenda rudi sala 5 zinapungua hadi kusalia sala 5 na hapo ndipo Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam alisema sasa anaona haya kurudi tena kwa Allah. Ila Allah Alimuambia kuwa ummah wako itasali sala 5 tu lakini Sisi tutamjaalia thawabu za sala 50.
Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah 
Kind Regards,
Muhammad KHATRI

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views