Ads 468x60px

Jun 2, 2014

Mi-iraj - PT 4 (Kiswahili)

Assalaamu alaikum,

Natumai hamjambo. Ingawa tumo ndani ya mwezi Sha-‘abaan lakini nataka nijitahidi nimalize risala yetu kuhusu msafara wa Isra na Mi-‘iraj.

Baada ya Kumshukuru Allah na kumtakia Rehma Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam, hapo juu ni aya ya kwanza ya Sura Bani Israil, ambayo inazungumzia msafara wa miraji.
Tafsiri ya aya:
Utukufu ni Wake Yeye Aliyempeleka Mja Wake katika sehemu tu ya usiku kutoka Msikiti wa Haraam (Makkah) hadi Msikiti wa Aqsa (Palestina), ambao umezungukwa na Baraka Zetu, ili Tumuonyeshe baadhi ya alama zetu. Hakika Allah ndiye Mwenye Kusikia Mwenye Kuona.
Leo tutazungumzia kuhusu jinsi gani watu walivyopinga muujiza huu tukufu.
Lau kama Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam angewaambia makafiri kuwa alipelekwa kuchupa mbingu 7, Arshi, Sidrah na Laa Makaan; bila shaka makafiri walijua nini kuhusu Arshi, Sidrah au Laa Makaan. Wanazuoni wanasema kuwa Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi wasallam alifahamisha makafiri kile ambacho ilikuwa akilini mwao na pia kile ambacho walikuwa wakishuhudia kila mara kuwa safari ya kutoka Makkah hadi Palestina ni wa siku ngapi? 
Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam aliporejea baada ya safari yake, ilikuwa usiku. Asubuhi yake walipokuja baadhi ya makafiri Msikitini, Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam aliwaambia kuwa Mola wake Alimpeleke hadi Msikiti wa Aqsa kutoka Msikiti wa Makkah katika sehemu fupi tu ya usiku. Makafiri wakasema: hivi hii inawezekana vipi na mara hii tu umerudi?
Makafiri walikuwa katika jitihada zao za kutafuta jambo lolote dhidi ya Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam ili wamdhalilishe. Wakaona hapa ndiyo Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam amepatikana kwa kuwapa taarifa hizo, kwani kwao ilikuwa ni jambo lisilowezekana ya mtu kusafiri umbali wote huo tena katika sehemu tu ya usiku!! Wakaanza propaganda zao. Ilishauriwa taarifa hizo zimfikie yule aliye karibu sana na Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam, ikiwa mtu huyo ataingiwa na mashaka juu ya safari hiyo, basi wengine wote watakuwa na mashaka. Wakafika nyumbani kwa Sayyidina AbuBakr Siddiq RadwiyAllahu Anhu. Ikumbukwe kuwa hadi muda huo, cheo cha siddiq alikuwa bado hajaipata.
Makafiri: Je umemsikia sahiba (Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam) amesemaje leo?
AbuBakr: Amesema nini?
Makafiri: Eti anadai amepelekwa Msikiti wa Aqsa kutoka Msikiti wa Makkah katika sehemu tu ya usiku na kuwe amesharudi! Je inawezekana hiyo?
AbuBakr: Je mmemsikia Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam kwa masikio yenu bila ya kuambiwa na mtu mwingine?
Makafiri: Ndiyo sisi tumemsikia hata na wewe pia ukamsikie.
AbuBakr: Ikiwa Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam amesema hivyo, basi mimi nashuhudia kuwa kweli Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam alipelekwa na kurudi pia.
Makafiri hawakuamini tamko la AbuBakr na hivyo mpango wao ulitimuliwa.
AbuBakr akaja kwa Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam na kutoa ushahidi kuwa wewe umesafiri kutoka Msikiti wa Makkah hadi Msikiti wa Aqsa na kurudi tena katika sehemu tu ya usiku. Ewe Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam hata ukisema kuwa umepelekwa hadi kuchupa mbingu 7 pia niko tayari kuamini. Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam akamwambia ewe AbuBakr na ndivyo ilivyo. Mimi nilipekwa Arshi, Peponi, Sidrah, Laa Makaan hadi kumkaribia Allah na kisha Allah Alinijaalia ufunuo (wahyi).
Baadhi ya watu walieneza uongo, baadhi walidanganyika. Eleweni kuwa msafara huu una sehemu 3.
1)Msafara wa kutoka Msikiti wa Makkah kwenda Msikiti wa Aqsa na kurudi. Makafiri walitaka waelezwe baadhi ya alama. Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam akasema alipokuwa anarejea aliona msafara mmoja ambao walipotelewa na ngamia wao, waliweka maji sehemu moja na mimi nikanywa.
Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam aliwapa habari za msafara mwingine kuwa una mali nyingi na kuwa itaingia Makkah kesho yake kabla ya jua kuzama. Pia nilipokaribia kuwasili Makkah nilikutana na msafara mwingine ambao utaingia kabla ya jua kuchomoza.
Makafiri walisambaza majasusi wao kujaribu kuhakiki ukweli wa kauli ya Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam. Kundi moja ilipelekwa kwenye kitongoji kimoja ili washuhudie kama kweli msafara unaingia muda wa kuchomoza jua!! Kweli, mara tu jua ilipochomoza na msafara ndiyo huo ukaingia.
Jitihada zao zikahamia kusubiri msafara wa kuingia muda wa jua kuzama. Msafara ulichelewa njiani na kwa maana hiyo ilikuwa ikawie kuingia. Wanazuoni wanaelezea hekima kuwa Allah Aliizuia jua hadi msafara ulipokaribia kuingia ndipo jua ikazama ili kusadikisha kauli tukufu ya Kipenzi Chake Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam. Makafiri wote hawakua na la kusema!!
Makafiri waliposhindwa, sasa walianza kumuuliza Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam; kama kweli ulienda Msikiti wa Aqsa basi utueleze Msikiti una madirisha mangapi, milango mingapi, ngazi ngapi?
Allah Alimuamrisha Jibrail auchukue Msikiti wa Aqsa na kuiweka mbele ya Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam. Mtume Muhammad Swall-Allahu Alaihi Wasallam akawa anawajibu kwa kila swali walilouliza.
Makafiri wote walidhalilika.
Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah,
Kind Regards,
Muhammad KHATRI

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views