Ads 468x60px

Jun 13, 2014

Nisf Sha'abaan (Kiswahili)

Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo. Ifuatayo ni risala fupi kuhusu fadhila za Nisf Sha-‘abaan, ambayo ni kesho usiku kuamkia Jumamosi.
LAYLATUL BARAA-I (USIKU WA KUWA HURU NA MOTO WA JAHANNAM NA PIA KASIMATU RIZKI):
Inaitwa usiku wa kuwa huru kwani ni usiku ambamo Waislamu huwa huru na moto wa jahannam. Pia ni usiku tukufu zaidi baada ya ule wa Laylatul Qadri. Ni usiku ambamo matukio yote ya mwaka unaokuja huandikwa, mfano: wepi watakufa, wepi watazaliwa, nani atapata rizki na kiasi gani, n.k.
Mtume Isa Alaihissalaam aliipenda jiwe zuri juu ya mlima, ambamo (ndani ya jiwe) aliishi Mcha Mungu aliye ndani ya ibada kwa miaka 400 na akila matunda kutoka mti uliopo ndani ya jiwe hili. Hata hivyo Mtume isa Alaihissalaam aliambiwa kuwa yeyote katika ummah wa mtume swallallahu Alaihi Wasallam akikesha ibada usiku huo, basi atapata thawabu zaidi ya ibada ya miaka 400 ya Mcha Mungu huyo. Sub-hanallah!!
Ni usiku ambamo Rehema ya Allah hushuka hadi mbingu ya kwanza na hunadi kwa wenye shida na matatizo na msamaha, n.k. Isipokuwa watu wa aina 10 watakuwa mbali na Rehema hiyo ya Allah usiku huo. Nao ni kama wafuatao:-
(1)  Mshirikina (2) Kafiri (3) Mchawi (4) Mnajumi (5) Mzinifu (6) Mlevi (7) Mshawishi
(8) Mwenye kupokea riba (9) Mwenye kuwaasi wazazi (10) Mfitini
Hata hivyo, ikiwa watu hao watatubu kwa moyo mkunjufu usiku huo na kuahidi kutorudia madhambi hayo, basi kwa Rehema ya Allah watasamehewa.
Allah Atulinde na maasi hayo, amin.
Ibada ya usiku huo huanza baada ya sala ya Maghrib, kwa rakaa 2 za Sunnah kisha Sura Yasin na Dua ya Nisf Sha-‘abaan. Hiyo inarudiwa mara tatu. Dua ya Nisf Sha-‘abaan ni hii ifuatayo:-
Maswali / maoni yanakaribishwa.

JazakAllah,
Kind Regards,
Muhammad KHATRI

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views

Follow by Email