Ads 468x60px

Apr 3, 2013

Fadhila za Elimu - PT 2‏ (Kiswahili)


Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo na mmeifuatilia sehemu ya 1 ya risala. Ifuatayo ni sehemu ya 2.

AYA: INNAMA YAKHSHALLAHA MIN IBAADIHIL ULAMAA. 
Tafsiri ya aya:
Hakika wamchao au wenye kumuogopa Allah zaidi katika viumbe vyake ni wanazuoni tu.
Kwani mimi na nyinyi hatumuogopi Allah? Sasa imekuaje hapa wakatajwa wanazuoni tu ni wenye kumuogopa Allah? 
HADITHI: Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam amesema kuwa kujifunza elimu ni jambo la lazima kwa kila Muislamu mwanamme na mwanamke. (Al Mishkat).
Tunajua kuwa haiwezekani kwa kila mmoja kuwa mwanachuoni, ila ni muhimu sana kwa kitongoji kuwa na mwanachuoni la sivyo wakazi wake wote watakuwa na madhambi. Ila kila Muislamu ni lazima aelewe masuala muhimu kama vile sala, zaka, saumu, nk.
HADITHI: Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam amesema kuwa muwe na njia 4 za kuishi na mkifuata ya 5 basi mtaangamia, nazo ni:-
1) Uwe mwanachuoni  AU 2) mwanafunzi   AU 3) mwenye kukaa pamoja na wanazuoni  AU 4) mwenye kuwapenda wanazuoni.
Jambo la tano litawaangamiza.
HADITHI: Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam amesema kuwa itakuja zama ambapo watu wataikimbia elimu  na wanazuoni.
HADITHI: Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam amesema kuwa itakuja zama ambapo elimu itaondolewa. (Maana yake kuwa wanazuoni wataondolewa, watu watawaendea majahili, ambao hawatakua na ujuzi wa halali na haramu, kuulizia masuala yao).
Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam akaendelea kusema kuwa Allah Atawaingiza watu hao katika matatizo matatu:-
1) Baraka ya riziki itaondolewa    2) Wataongozwa na viongozi madhalimu
3) Mauti itawajia hali ya kuwa imani imewatoka.

Maswali / maoni yanakaribishwa.
 JazakAllah,
 Kind Regards,
 Muhammad KHATRI 

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views