Ads 468x60px

Apr 10, 2013

Fadhila za Elimu - PT 3 (Kiswahili)

Assalaamu alaikum,
 Natumai hamjambo. Hivi mnakumbuka hadi sasa imeelezwa nini kuhusu fadhila za elimu? Tunaendelea …

AYA: INNAMA YAKHSHALLAHA MIN IBAADIHIL ULAMAA.
 Tafsiri ya aya:
Hakika wamchao au wenye kumuogopa Allah zaidi katika viumbe vyake ni wanazuoni tu.

Kwani mimi na nyinyi hatumuogopi Allah? Sasa imekuaje hapa wakatajwa wanazuoni tu ni wenye kumuogopa Allah?
Baada ya kuelewa faida na fadhila ya elimu kwa ufupi, hebu tuangalie kwa jinsi gani Masahaba na wazuoni walivyojitolea maisha yao na matatizo waliyoyapata ili mradi tu watuwekee sawa masuala ya dini yetu.
Hadithi hii ipo ndani ya Kitabu cha Al Mishkat, Mlango wa Elimu, ameipokea riwaya Kasir bin Qais RadwiyAllahu Anhu. Sahaba wa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam, Abu Dardah RadwiyAllahu Anhu – ni miongoni mwa Masahaba wanachuoni (kwa maana walikuwa wakiwafundisha dini Masahaba wenzao). Baada ya Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam kuiaga dunia, Abu Dardah nae aliihama mji wa Madina kwenda Damascus, Syria. Huko alikuwa akitoaga darsa za Hadithi ndani ya Msikiti mkuu wa Ijumaa. Kasir anaelezea kuwa siku moja walikuwa katika darsa zao, mara akaja mtu na kumuendea moja kwa moja Abu Dardah. Akamwambia “ewe Abu Dardah, hivi unajua kuwa mimi nimetoka umbali wa mji wa Madina na kilichonileta hapa si kingine labda ukafikiria pengine nimeleta bidhaa kutoka Madina kuuza hapa au pengine nitanunua bidhaa kwenda kuuza Madina, hapana! Mimi nimepata taarifa huko Madina kuwa kuna Hadithi moja ya Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam ambayo ni wewe tu pekee uliyepokea riwaya, ndiyo nimekuja kuisikia”.
Sub-hanallah!! Hivi kweli leo tunaweza kuwapata watu wenye kuwa na uchungu wa elimu kiasi hicho?? Bila shaka hapana!!
Abu Dardah RadwiyAllahu Anhu akamsimulia hiyo Hadithi: nimemsikia Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam akisema kuwa yule anaetoka kutafuta elimu (ya dini) basi huwa kwenye njia za Peponi, Malaika hutanda mbawa zao juu yake kumfanyia kivuli (riwaya nyingine inasema hutanda mbawa chini ya miguu yake), kisha wanyama wote wa ardhini – hata sisimizi ndani ya tundu, ndege wote wa angani na samaki wote wa baharini humuombea mtu huyo. Kisha akasema kuwa fadhila ya mjuzi juu ya mwenye kufanya ibada ni kama fadhila ya mwezi wa usiku wa 14 juu ya nyota zote (riwaya nyingine inasema kuwa fadhila ya mjuzi juu ya mwenye kufanya ibada ni kama fadhila yangu juu ya mtu mdogo sana miongoni mwenu”. 
Tuelewe kuwa enzi hizo usafiri uliotumika ni kumpanda ngamia – hapakuwa na mabasai, magari, reli wala ndege! Ila Waislamu walikuwa na moyo sana wa kujifunza na kueneza elimu.

Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah,
Kind Regards,
Muhammad KHATRI

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views