Ads 468x60px

Apr 17, 2013

Fadhila za Elimu - PT 4 (Kiswahili)


Assalaamu alaikum,
 Natumai hamjambo. Nashindwa kabisa kupata picha kama mada hii mnaifuatilia kwa makini ama mnaboreka!! Maana hakuna aliuliza hadi hivi sasa!! Haya tunaendelea …
 AYA: INNAMA YAKHSHALLAHA MIN IBAADIHIL ULAMAA.
 Tafsiri ya aya:
Hakika wamchao au wenye kumuogopa Allah zaidi katika viumbe vyake ni wanazuoni tu.
 Sahaba mwingine wa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam, AbdulRahman RadwiyAllahu Anhu, alitoka nyumbani kwake na alirudi baada ya miaka 28. Alipotoka, alimuacha mkewe mja mzito na hivyo kumuachia pesa yenye thamani ya dinari 40,000 (ni zaidi ya mamilioni kwa thamani ya sasa). Baada ya mkewe kujifungua na kumlea mwanae, alimsomesha hadi akawa mjuzi mkubwa sana wa kutoa darsa za Hadithi ndani ya Msikiti Mtukufu wa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam. AbdulRahman aliporudi na kumuona mwanae alivyokuwa mjuzi, alifurahi sana na kumshukuru Allah.
 Madhumuni ya kusimulia kisa hapo juu ni kuwa enzi hizo, hata kina mama walikuwa na shauku kubwa ya kuwafundisha watoto wao; kinyume kabisa na hali tuliyonayo sasa!
 Wanazuoni walijitolea maisha yao yote kwa ajili ya elimu tu. Imam Muslim, mtunzi mmojawapo kati ya 6 wa vitabu vya Hadithi, aliposikia Hadithi fulani katika darsa mmojawapo, akawa na shaka na aidha aliyepokea riwaya au daraja ya hadithi hiyo. Akajifungia chumbani kwake kutafuta Hadithi iliyozungumzwa. Kila kitabu akichambua Hadithi hiyo haioni na mara akasikia njaa. Akaona ni kupoteza muda kama akienda kula na hivyo alichukua debe la tende (lenye kilo sijui 10, 15 au 20) na kuiweka karibu. Huku anakula tende na huku anaitafuta hiyo Hadithi. Alishtukia tende zimeisha na kutokana na kula nyingi mno mauti ukamkuta hapo.
 Sakaratul maut (machungu ya muda wa mwisho kabla ya kutolewa roho) ni wa mtihani mkubwa sana kwa sisi Waislamu. Kwani imeelezwa kuwa shetani anajitahidi sana kumyumbisha mja ili tu akufuru na kifo kimkute hali ya kuondokewa na imani. Pia imeelezwa kuhusiana na uchungu huo kuwa mtu akipigwa bakora 150 (na riwaya nyingine inasema bakora 1,000) uchungu wake ni mdogo kuliko uchungu wakati wa kifo!! Ndiyo maana Mama Aisha aneleza kuwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam katika siku zake za mwisho aliweka ndoo ya maji karibu nae kisha alilowesha mkono wake na kuifuta usoni mwake na kusema “uf sakaratul maut”! (yaani uchungu wa kifo) Allah Aturehemu na aturahisishie uchungu huo, amin.
Abdullah bin Umar RadwiyAllahu Anhu (Sahaba wa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam) alipokuwa katika sakaratul maut, aliulizwa kuwa anatamani kitu gani kabla ya kuondoka hapa duniani. Wengi wetu tunatamani mambo ya kudia pengine sikufanikiwa na hili au lile, n.k. Sub-hanallah!! Sahaba huyo akajibu kuwa “wallahi natamani sana nifundishwe kile ambacho sijajifunza”.

Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah,
Kind Regards,
Muhammad KHATRI

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views