Ads 468x60px

Apr 30, 2013

Sayyidina Abu Bakr Siddiq - PT 1‏ (Kiswahili)


Assalaamu alaikum,
 Natumai hamjambo. Kama nilivyoandika katika risala iliyopita kuwa huu ni Mfungo 9 (Jamadi-ul-Akhar) na mwezi 22 Khalifa wa kwanza wa Kiislamu, Sayyidina Abu Bakr RadwiyAllahu Anhu aliiaga dunia hii.
 Ifuatayo ni sehemu ya kwanza ya risala kuhusu maisha ba fadhila zake kwa muhutasari.
AYA:  THANIYATHNAINI IDH HUMA FIL GHAARI IDH YAQULU LISWAHIBIHI LAA LAH-ZAN INNALLAHA MA-ANA.
 Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam, hapo juu ni aya kutoka Sura Tawba inayoelezea fadhila mmojawapo ya Khalifa wa 1 wa Kiislam, Sayyidina AbuBakr Siddiq.
TAFSIRI: Wakati wawili (Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam na Sy AbuBakr) walipokuwa ndani ya pango, mmoja alimuambia mwenzake usihuzunike, hakika Allah yuko pamoja nasi.
 Jina lake hasa ni Abdullah, ila AbuBakr likawa maarufu na Siddiq alipewa na Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam kwa kusadikisha msafara wa Miiraj. AbuBakr kamwe hakuabudu masanamu hata kabla ya kusilimu wala hakuwahi kunywa pombe kipindi bado haijaharamishwa; na alisema hawezi kutumwa kinywaji kinachoua akili ya binadamu. Baada ya kuwa na uwezo kutembea, baba yake (Abu Quhafa) alimpeleka mbele ya sanamu na kumuambia kuwa huyu (sanamu) ndiye mungu wetu anaetulisha, visha na kutupa kila kitu. Sy AbuBakr akasimama mbele ya sanamu na kusema: mimi nina njaa nilishe, nina kiuu ninyweshe, sina nguo nivishe. Alipoona kimya, alichukua jiwe na kulipiga sanamu na ikaanguka. Baba yake alikasirika sana na kumpiga kibao kisha kumburuza hadi nyumbani na akamwambia mkewe : hebu mfundishe mwanao, leo kampiga mungu wetu, hana adabu huyo. Mkewe alimjibu: ewe Abu Quhafa, naomba usimwambie chochote huyu mwanetu, kwani nilipomzaa nilisikia sauti ikisema: umebarikiwa mtoto atakaekuwa rafiki wa karibu wa Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam, Mtume wa mwisho. Mimi simjui huyu Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam ni nani.

Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah,
Kind Regards,
Muhammad KHATRI 

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views