Ads 468x60px

May 15, 2013

Rajab PT 2 (Kiswahili)


Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo. Kabla ya kuendelea na masimulizi ya mwezi Rajab, ndugu yetu mmoja ameuliza swali kama ifuatayo:- 
SWALI: Sheikh naomba kuuliza swali.Hivi Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam kabla hajaaga Dunia alikuwa ameshapanga silsila ya uongozi? Yaani labda Sayyidna Abubakar, then Sayyinda Omar ……..?
JIBU: Mtiririko wa uongozi baada ya Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam kuiaga dunia hii unaitwa KHULAFA-UR-RAASHIDIN (yaani Makhalifa wa kweli). Muongozo huo unapatikana katika aya MUHAMMADUR RASULULLAH, WALLADHINA MA-‘AHUU ASHIDDAA-U ALAL KUFFAARI RUHAMAA-U BAINAHUM TARAHUM RUKKA-AN SUJJADA …. (Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam ni Mjumbe wa Allah, na wale walio pamoja nae (anamaanishwa Sy AbuBakr Siddiq) na wakali kwa makafiri (anamaanishwa Sy Umar), lakini ni wenye huruma baina yao (anamaanishwa Sy Uthman) na utawaona wako katika kurukuu na kusujudu (anamaanishwa Sy Ali) …
Isitoshe Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alimuidhinisha Sy AbuBakr Siddiq kuwasalisha Masahaba wakati (Mtume) alipokuwa mgonjwa.

Na sasa masimulizi ya mwezi Rajab ..
Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam amesema kuwa Rajab ni mwezi wenye fadhila nyingi, thawabu ya amali njema huwa maradufu ya thawabu ya kawaida. Mwenye kufunga swaum 1 ndani ya Rajab, basi ni sawa na kufunga mwaka mzima.
 Siku 1 Mtume Isa Alaihissalaam alipokuwa akipita karibu na mlima mmoja, aliona nuru sehemu Fulani ya mlima. Alimuomba idhini Allah ili aweze kuzungumza na mlima. Mlima ilimuuliza nini atakacho?  Mlima ikasema kuwa ndani yake kuna Mcha Mungu mmoja nan i kwa sababu ya huyo mlima una nuru. Mtume Isa Alaihissalaam alimuomba Allah aonyeshwe huyo mtu na mara mlima ikapasuka na akaonekana Mcha Mungu aliye mzuri sana. Alisema kuwa yeye ni katika watu wa Mtume Musa Alaihissalaam na alimuomba Allah Amjaalie maisha marefu ili aweze kushuhudia zama za Mtume wa mwisho Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam na hivyo ahesabiwe miongoni mwa ummah wa Mtume wa mwisho. Mcha Mungu huyo alikuwa mlamani humo kwa miaka 600. Kisha Mtume Isa alimuuliza Allah kama kuna Mcha Mungu ardhini zaidi ya huyo bwana? Allah alimjibu: “Ewe Isa, lau kama mja wangu katika ummah wa Mtume wa mwisho akifunga siku moja tu ya mwezi Rajab, basi huyo mja kwangu atakuwa Mcha Mungu zaidi kuliko huyo bwana!! (SUB-HANALLAH). 
Baadhi ya tarehe muhimu:
Tarehe 4: Imam Shafi aliaga dunia. Jina lake ni Muhammad bin Idris na kizazi chake cha 4 kinakutana na kile cha Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam kwa Abdi Manaf. Amezaliwa mwaka 150 hijria na kufariki mwaka 204h mjini Cairo, Misri. Alikuwa akikhitimisha msahafu mmoja kila siku katika mwezi Ramadhani. Kila alipopatwa tatizo, basi huenda kuizuru kaburi la Imam Abu Hanifa na kisha huomba dua akimtawassul.
Tarehe 6: Walii mkubwa wa Allah Moinuddin Chishti aliaga dunia nchini India. Walii huyo alikuwa mwaka sambamba na Sheikh Abdul Qadir Jilani Qaddasallahu Sirrah. Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam alimjaalia uwalii wa bara hindi. Mabaniani milioni 9 walisilimu kwa jitihada zake.
Tarehe 10 Mtume Nuh na wafuasi wake walianza safari katika meli kabla ya tufani kali iliyowaangamiza waliompinga.
Tarehe 27: Msafara wa Isra na miraj ya Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam ambayo insha Allah tutaanza kuizungumzia hapo baadae.

Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah,
Kind Regards,
Muhammad KHATRI

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views