Ads 468x60px

May 10, 2013

Sayyidina Abu Bakr Siddiq - PT 4 (Kiswahili)


Assalaamu alaikum,
 Natumai hamjambo. Namilizia masimulizi ya Sayyidina Abubakr Siddiq RadwiyAllahu Anhu na nadhani imetupa picha fulani kuhusu jinsi gani alivyojitolea kwa ajili ya Allah na Mtume wake Swallallahu Alaihi Wasallam. 
Alichaguliwa Khalifa wa Kiislamu kwa kura zote za Masahaba wote akiwemo Sayyidina Ali RadwiyAllahu Anhu, aliyekiri kuwa yule aliyechaguliwa na Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam kuiongoza umma katika sala (imamu), basi bila shaka anapaswa kuwa Khalifa wetu. Ieleweke kuwa mwenye kupinga Usahaba wa AbuBakr, basi bila shaka anazikataa aya za Quran Tukufu na kwa hali hiyo atajiondoa katika Uislam.
 Sayyidina AbuBakr alikuwa mjasiri na shupavu sana kiasi cha kwamba wakati wa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam kuiaga dunia, baadhi ya mambo magumu yalijitokeza lakini aliyatatua kwa ujasiri mkubwa. Mmojawapo ikiwa: Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alituma jeshi la Masahaba shupavu na bado walikuwa ndani ya kitongoji cha mji wa Madina wakati Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alipoiaga dunia. Baadhi ya Masahaba walipomuomba Sayyidina AbuBakr kurejesha jeshi hilo ili kukabiliana na vurugu ikiwa zitatokea, alikataa kwa madai kuwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alishaituma jeshi hilo na hivyo yeye hawezi kuirejesha.
 Pia baadhi ya Masahaba walikataa kutoa zaka baada ya tume Swallallahu Alaihi Wasallam kuiaga dunia, lakini Sayyidina AbuBakr kwa ujasiri wake alihakikisha kila mstahiki wa kutoa zaka anatekeleza amri hiyo hata kama ikibidi kukabiliana nao kwa jihad.
 Bado hali ilikuwa haijatulia vizuri, mara akajitokeza Musailm bin Kazzaab aliyedai utume. Wafuasi wake walifikia 100,000 dhidi ya jeshi la Waislam kiasi cha 10,000; Waislam walishinda vita hivyo.
 FADHILA: Ingawa Sayyidina Abu Bakr Siddiq Radwiyallahu Anhu alikuwa mtu mwenye fadhila nyingi, lakini pamoja na yote hayo, kubwa zaidi ni kuwa vizazi vyake vinne (4) walikuwa Masahaba.  1 – Yeye mwenyewe Radwiyallahu Anhu.   2 – Baba yake, Abu Quhafa Radwiyallahu Anhu.    3 – Mwanae, AbdulRahman Radwiyallahu Anhu     4 – Mjukue, Abu Atiq Muhammad Radwiyallahu Anhu.
 Baadhi ya mambo muhimu ya Sayyidina Abu Bakr Siddiq Radwiyallahu Anhu alikuwa wa kwanza:
1 – Kusilimu.
2 – Kukiita Quran Tukufu “MSAHAFU” (Kitabu).
3 – Kuikusanya Quran Tukufu baada ya Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam.
4 – Kupigana na makafiri
5 – Kuwa Khalifa
6 – Khalifa aliyeanza ukhalifa katika uhai wa baba yake.
7 – Kumchagua Khalifa atakaemfuata.
8 – Kujenga hazina.
9 – Kuitwa Khalifa.
10 – Kujenga Msikiti miongoni mwa Waislamu.
11 – Miongoni mwa wafuasi wa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam kuingia Peponi.
 Kuhusu fadhila za Sayyidina Abu Bakr Siddiq Radwiyallahu Anhu, kuna aya nyingi za Quran Tukufu na Hadithi pia; kati ya hizo Hadithi 181 zimepokelewa katika fadhila zake tu, Hadithi 88 zimepokelewa na Sayyidina Abu Bakr & Sayyidina Umar bin Khattab Radwiyallahu Anhuma, 17 zimepokelewa na Abu Bakr, Umar & Uthman bin Affan Radwiyallahu Anhum, 14 zimepokelewa na Makhalifa wote wanne, 16 zimepokelewa na Makhalifa wote wane pamoja na Masahaba wengine. Hivyo, katika jumla ya Hadithi 316, Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam ametuthibitishia fadhila ya sahiba wake wa pango, Sayyidina Abu Bakr Siddiq Radwiyallahu Anhu.
Imani ina matawi 360 na Sy AbuBakr alijaaliwa matawi yote. Siku ya Qiyama, kila atakaeingia Peponi, ataitwa kupitia mlango maalumu kutokana na alivyo kithirisha ibada fulani; mfano kama mtu alikithirisha sana saumu, basi ataitwa kupitia mlango wa wenye kufunga saum. Sy AbuBakr ataitwa kupitia milango yote, inamaanisha alikuwa mkamilifu wa kila ibada.

Maswali/ maoni yanakaribishwa.
JazakAllah,
Kind Regards,
Muhammad KHATRI 

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views