Ads 468x60px

May 6, 2013

Sayyidina Abu Bakr Siddiq - PT 3‏ (Kiswahili)

Assalaamu alaikum,

Natumai hamjambo. Tunaendelea na masimulizi ya Sayyidina Abubakr Siddiq RadwiyAllahu Anhu.

Sy Abubakr hakuabudu sanamu wala kunywa pombe, kabla ya kusilimu, na katika enzi ambazo ilikuwa haiajaharamishwa na kusema kuwa pombe inaua akili ya binadamu kwa hiyo sikuona sababu kuitumia ambapo inanipa hasara tu!

Sy Abubakr alikuwa karibu sana na Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam kila mara. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam amesema kuwa kila aliyempa wito wa Uislamu, kwanza alikataa isipokuwa Sy Abubakr aliyekubali mara moja.

Sy Abubakr ndiye aliyemkomboa Bilal bin Rabah kwa pesa nyingi mno pale alipoteswa kwa sababu ya kusilimu.

Sy Abubakr alipofuatana na Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam kutoka Makkah kuhamia Madina, njiani alimbeba Mtume mgongoni na kutembea juu ya vidole vya mguu kwa kuhofia makafiri wasije kuyafuata vikanyago. Walipojipumzisha kwenye pango, Sy Abubakr aliingia kwanza kuisafisha na kuziba matundu yote, kisha ikabaki tundu moja tu, aliloziba kwa kidole cha mguu. Kumbe ndani alikuwa nyoka wa zama za Mtume Musa aliyetaka kumuona Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam. Aliposhindwa kupita kwenye matundu, ndipo alimng’ata Sy Abubakr. Kwa kuwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam aliweka kichwa chake kitukufu kwenye paja la Sy Abubakr na alilala, Sy Abubakr alivumilia sana maumivu makali ya kung’atwa na nyoka na wala hakutikisika. Ila machozi yalibubujika kwenye uso tukufu wa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam na ndipo Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam aliamka na kufahamishwa hali halisi. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alimpaka mate yake matukufu Sy Abubakr sehemu alipong’atwa na maumivu yalitoweka.

Wakati wa ugonjwa wake, Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alimsimamisha kwenye nafasi yake Sy Abubakr kuwa Imamu wa Masahaba.


Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alipoaga dunia, Masahab walichangayikiwa kabisa na Sy Umar alitembea na panga akisema “yeyote atakaesema kuwa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam ametuondoka, basi nitamuua”. Lakini Allah Alimjaalia ushupavu Sy Abubakr, alipoingia Msikitini na kuanza kuwatuliza Masahaba, kisha alisimama juu ya mimbar. Alisoma aya ya 144 ya Sura Aali Imran : na Muhammad hakuwa ila ni Mtume. Na wamekwishapita kabla yake Mitume, je akifariki na kuuawa basi mtageuka kurudi nyuma? Na atakaegeuka kurudi nyuma, huyo hatamdhuru kitu Allah. Na Allah Atawalipa wanaomshukuru. Baada ya kumaliza aya hiyo ndipo Masahaba walitulia.


Maswali/ maoni yanakaribishwa.

JazakAllah,

Kind Regards,

Muhammad KHATRI

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views