Ads 468x60px

Nov 11, 2013

Hijrah (Kiswahili)


Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo. Ifuatayo ni risala fupi kuhusu hijrah – kuhama kutoka Makkah na kwenda Madina.
Kalenda yetu pia huanzia mwenzi wa hijrah na ndyo maana inaitwa HIJRIYYAH. Ingawa mwaka wetu wa 1435h  haumaanishi kuwa safari hiyo ya hijrah imetimiza miaka hiyo, la, bali kalenda ilianziwa baada ya muda Fulani. 
AYA:  THANIYATH NAINI IDH HUMA FIL GHAARI IDH YAQULU LISWAHIBIHI LAA TAHZAN INNALLAHA MA-‘ANA.
Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi wasallam, sehemu ya aya hapo juu ya 40 kutoka Sura Tawbah (9), inazungumzia msafara wa hijrah.
TAFISIRI: … naye ni wa pili katika wawili walipokuwa katika pango, naye akamwambia sahibu wake: usihuzunike, hakika Allah yuko pamoja nasi …
Dhulma dhidi ya Waislamu ilipokithiri, Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alihukumiwa kuihama mji wa Makkah na kwenda Madina. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alimkabidhi amana za watu Sy Ali na kumwambia awalipe, kisha alale kwenye kitanda cha Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam na kesho yake aje Madina. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alitoka na Sy AbuBakr. Kwa kuwa makafiri walipata taarifa ya kuhama kwa Mtume, walikaa nje ya nyumba wakimsubiri kumuua. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alitoka akisoma aya ya Sura Yasin, akachukua mchanga na kuwamwagia kichwani na wale wote wakalala usingizi na Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam akapita.
Sy AbuBakr alimbeba Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam mgongono mwake na mwenyewe akatembea juu ya viganja vya miguu ili maadui wasitambue vikanyago. Walipofika kwenye pango THOUR, Sy AbuBakr aliingia ndani kuisafisha na kisha kumuita Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam. Sy AbuBakr alifunga matundu yote ila moja tu ikabaki. Nyoka aliyekuwepo hapo tangu zama za Mtume Musa kutaka kumuona Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam, alishindwa kutoka na hivyo alimng’ata Sy AbuBakr kwenye mguu. Sy AbuBakr alivumilia maumivu na machozi yalipobubujika kwenye uso wa Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam ndipo Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alimwekea Mate matukufu na alipona.
Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam alipowasili Madina alipokewa kwa shangwe na Qasida. Pia alijenga Msikiti mjini hapo.
Maswali / maoni yanakaribishwa.
JazakAllah,
Muhammad KHATRI

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views

Follow by Email