Ads 468x60px

Jun 6, 2013

ISRA NA MI-'IRAJ - PT 4‏ (Kiswahili)

Assalaamu alaikum,
Natumai hamjambo. Natumai mnakumbuka tulipoishia katika risala yetu ya Mi-‘iraj. Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam katika safari yake kuelekea mbinguni hadi kufika mbingu ya 7; tunaendelea.
 AYA: THUMMA DANAA FATADALLA. FAKAANA QAABA QAUSAINI AU ADNAA. FA-AWHAA ILAA ABDIHI MAA AWHAA.

Baada ya kumshukuru Allah na kumtakia Rahma Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam, aya hapo juu ni ya 8 HADI 10 ya Sura An Najmi, inayozungumzia Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam kuonana na Allah.
Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam alishuhudia Pepo na moto na baadae kufika Sidrah, ambapo alisikia sauti ya SUB-HANALLAH, ALHAMDULILLAH. Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam aliuliza ni kitu gani hiyo? Jibrail akajibu kuwa Sidrah, ambayo ni mti mkubwa, Malaika huleta dhikri. Hapo ndipo tamati ya Malaika. Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam alimwambia Jibrail waendelee lakini Jabirail akamjibu kuwa akisogea hatua moja kutoka hapa basi mbawa zake zitaungua kutokana na Nuru ya Allah; akamuambia Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam aendelee na safari.
Hapa ndipo Jibrail alimuomba idhini Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam ili amuonyeshe utukufu aliojaaliwa na Allah; kwani siku zote hizo Jibrail alikuwa akimjia Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam katika sura ya binadamu tu. Jibrail alipoondoa pazia mbawa zake 600 zikaonekana na ukubwa wa kila mbawa ulizidi hata ukubwa wa ardhi yote ya dunia. Wanazuoni wanasema lau kama Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam angemuonyesha utukufu wake, basi Jibrail angezimia pengine hadi kiyama.
Baada ya hapo Jibrail alimuomba Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam amtakie idhini kutoka kwa Allah kuwa siku ya kiyama wakati umma wake utakapopita kwenye njia nyepesi, basi yeye atande mbawa zake kuwasalimisha wapite kwa raha.
Baada ya hapo Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam alimpanda Rafraf na kuelekea juu zaidi. Baada ya kupita Arshi ndipo alimuona na Allah kwa macho yake, na hapo ndipo alimkaribia Allah. Kisha Allah Alimjaalia wahyi. Allah Alimuuliza je umeleta nini?
Mtume : Attahiyatu lillahi wasswalawaatu wattayyibaatu.
Allah : Assalaamu alaika ayyuhan Nabiyyu warahmatullahi wabarakaatuhu (salamu ziwe juu yako ewe Mtume pamoja na Rahma na Baraka).
Mtume : Assalaamu alaina wa-alaa ibadillahis swaalihin (salamu ziwe juu yetu na waja wako wema).
Hapo ndipo Allah Alimzawadia sala 50 za kutwa nzima. Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam alianza safari ya kurudi, lakini alipokutana na Mtume Musa katika mbingu ya 6, alimuambia arudi kwa Allah ili zipunguzwe kwani ummah wake walifaradhishiwa sala 2 tu kutwa nzima na walishindwa. Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam alirudi tena kwa Allah kutaka kupunguziwa, na Allah alimpunguzia sala 5. Alipofika tena kwa Mtume Musa, aliambiwa bado ni nyingi na kurudi tena kwa Allah. Kila nenda rudi sala 5 zinapungua hadi kusalia sala 5 na hapo ndipo Mtume Muhammad Swallallahu Alaihi Wasallam alisema sasa anaona haya kurudi tena kwa Allah. Ila Allah Alimuambia kuwa ummah wako itasali sala 5 tu lakini Sisi tutamjaalia thawabu za sala 50.
 Wanazuoni wanasema kuwa Miraji ya Mtume Swallallahu Alaihi Wasallam ni kuonana na Allah, na ya Waislamu ni kutekeleza sala 5 kutwa nzima.

Kuna ndugu yetu mmoja kauliza hivi:-
SWALI: ningependa kujua kuhusu sala endapo sala imekupita kisha wataka ilipa baada ya muda wake kupita ni sawa? na je unapoilipa unasali rakaa zote kama sala ilivo ama inakuwaje?
JIBU: Kwanza kabisa naomba ieleweke kuwa sala yoyote ikipita (kwa maana ya kuikosa), basi hiyo itabaki kuwa ni deni hadi ilipwe; iwe sala ya leo, jana au hata ya miaka iliyopita – bado ni deni. Hivyo sala hiyo (au hizo) zilipwe haraka iwezekanavyo; kwa maana ya kusali kama sala husika iliyopita.
Utaratibu wake ni kama tunavyosali sala zetu, hivyo itasaliwa ipasavyo.
Kwa mtu anaetaka kulipia sala zake za miaka iliyopita; aidha alipie sala zote za wakati mmoja hadi ziishe (mfano awe anazilipia sala ya Alfajir tu hadi zinaisha, kisha anahamia sala ya Adhuhuri, n.k.) au anasali sala za siku kwa mtiririko wake (mfano Alfajiri kisha Adhuhuri, n.k). Kumbuka kuwa kuna rakaa 20 kwa siku na ni Faradhi tu za kulipia pamoja na Witri.
Natumai nimeeleweka.
Maoni / maswali yanakaribishwa.
JazakAllah,
Muhammad KHATRI 

0 comments:

Post a Comment

Enter your Comment here...

 

Visitor's Traces

Total Page views